array(0) { } Radio Maisha | Idadi ya viongozi wanaopinga ripoti ya sensa inaendelea kuongezeka
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Idadi ya viongozi wanaopinga ripoti ya sensa inaendelea kuongezeka

Idadi ya viongozi wanaopinga ripoti ya sensa inaendelea kuongezeka

Idadi ya viongozi wanaopinga ripoti ya sensa iliyotolewa mapema wiki hii inaendelea kuongezeka huku wakisisitiza kwmaba data iliyotolewa si halali.

Gavana wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo amesema kwamba ripoti  iliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Takwimu nchini KNBS inaonesha  kwamba idadi ya watu kwenye kaunti ya Pokot Mgaharibi ilipungua kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Lonyangapuo amesema idadi ya watu elfu mia tisa ishirini na moja mia mbili arubaini na moja iliyotolewa si halali kwani kulingana na serikali iyo hiyo ya Kitaifa ni kwamba, Kaunti ya Pokot Magharibi inaongoza katika idadi ya kina mama wanaojifungua ikilinganishwa na kaunti nyingine.

Viongozi wengine ambao wameipinga ripoti hiyo ni wale wa maeneo ya Kaskazini Mashariki ambao wametishia kuwasilisha kesi mahakamani.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa wanadai kuna njama ya kuyanyima baadhi ya maeneo fedha ndio maana kuna idadi ndogo ya watu iliyorekodiwa katika ripoti hiyo ya sensa. Aidha inadaiwa kuwapo kwa njama ya kuyaondoa baadhi ya maeneo bunge kwa kutumia data hiyo.