array(0) { } Radio Maisha | Ngunjiri vikali ripoti iliyowasilishwa bungeni kuhusu Uwanja wa Ruringu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ngunjiri vikali ripoti iliyowasilishwa bungeni kuhusu Uwanja wa Ruringu

Ngunjiri vikali ripoti iliyowasilishwa bungeni kuhusu Uwanja wa Ruringu

Mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu amepinga vikali ripoti iliyowasilishwa bungeni kuhusu kiwango cha fedha zilizotumika katika ujenzi wa Uwanja wa Ruringu kuwa shilingi milioni mia moja huku akisema kuwa ujenzi huo haukutumia kiwango hicho.

Akizungumza alipozuru uwanja huo ambapo ujenzi unaendelea, mbunge huyo amemtaka mwanakandarasi anayeendesha mradi huo kuwajibika kwa kuwa ripoti hiyo si sahihi. Amesema huenda fedha hizo zilifujwa.

Wambugu aidha amesema kuwa asilimia thelathini na tatu iliyowekwa kuonesha kiwango cha ujenzi kilichokamilika ni ya uongo kwani ujenzi kwenye uwanja huo ulisitishwa.

Uwanja wa Ruringu ni mmoja kati ya viwanja vilivyoahidiwa kujengwa kwa viwango vya kimataifa na Serikali ya Jubilee wakati wa kampeni za mwaka wa 2013.