array(0) { } Radio Maisha | ''Samahani mashabiki kwa kushindwa na Mathare- lakini AFC Leopards watakiona'' ameahidi Pollak
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

''Samahani mashabiki kwa kushindwa na Mathare- lakini AFC Leopards watakiona'' ameahidi Pollak

''Samahani mashabiki kwa kushindwa na Mathare- lakini AFC Leopards watakiona'' ameahidi Pollak

Mkufunzi wa Gormahia Steven Pollack ametia usena katika shamra shamra za debi la mashemeji kwa kuwaahidi mashabiki wa K’ogallo ushindi.

Akizungumza na Redio Maisha mapema Ijumaa baada ya mazoezi yao katika uwanja wa Camp Toyoyo, Pollack alionesha ujasiri.

“Nimecheza mechi nyingi za watani barani Afrika na maishani nikiwa mchezaji. Mechi hii kwangu mimi japo ni debi la kwanza, lakini naichukulia kama yeyote ile. Maajuzi dhidi ya Mathare United tuliteleza, lakini hatujaanguka. Jumapili lazima tushinde. Mashabiki wetu nawaomba msamaha kwa kupoteza dhidi ya Mathare lakini jumapili wajitokeze na waoneshe uzalendo wao kwa Gormahia.” Alihimiza Pollack huku akiongezea kwamba misukosuko ya hela na kutatizika kiuchumi kwa wachezaji wake ni jambo ambalo liko nje ya uwezo wake.

Siku ya jumatano jioni, Mathare united iliwafunga Gormahia bao moja bila jawabu katika mechi ya ligii kuu nchini KPL.

Tetesi kutoka kambi ya ‘wuod Ogallo’, maanake nyumba ya Ogallo, ambayo ndiyo kitovu cha washika dau wote wa ndani kwa ndani wa mabingwa hawa wa KPL mara 18, niza kusikitisha. Penyenye ni kwamba wachezaji wa Gormahia hawajalipwa mishahara takriban miezi miwili sasa. Kabla ya mechi yao dhidi ya Mathare, kulishuhudiwa pia mgomo. Siku ya jumatano, wachezaji takriban sita pekee ndio walihudhuria mazoezi.

“ Najua kuna shida ya hela Gormahia na hata katika vilabu vingine kote kote nchini pia. Hata ligii kuu nchini KPL pia haina hela. Ni vigumu pia kujaribu kuwapa motisha wachezaji hawa ilhali hali yao ya uchumi si nzuri. Lakini tunajaribu tuwezavyo, jumapili ni siku kubwa kwetu sote wana K’ogallo. Kwa hivyo lazima tujitokeze kwa fujo ili tushinikize ushindi” Alimalizia Pollack.

Gormahia sasa iko katika nafasi ya pili nyuma ya Tusker fc baada ya kucheza mechi sita na alama 15. Tusker ambayo inafunzwa na gwiji Robert Matano, wako kidedea na alama 16 baada ya mechi nane. Ikumbukwe ya kwamba K’ogallo wana mechi mbili mkononi kwa sababu walikuwa wanashiriki michuano ya mashirikisho barani Afrika. Katika michuano hiyo, wali banduliwa nje na Daring Club Motema Pembe ya taifa la kidemokrasia la Congo.

Sasa macho yote, hisia, akili na ubongo zita elekezwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani. Gormahia ndio itakayo kuwa timu ya nyumbani. Wafuasi wa K’ogallo wana imani ya kwamba timu yao itaendeleza matokea mazuri waliyoyapata msimu jana walipowapiga Ingwe nyumbani 2-0 na ugenini 3-1.

Ikumbukwe pia Afc leopards haijawahi shinda Gormahia tangu mwaka wa 2016. Watani hawa wajadi walikutana mara ya kwanza mwezi Mei, tarehe tano, 1968. Gormahia ilishinda mechi hiyo 2-1. 

Ubabe huu wa Gormahia ulianza zama zile, tusubiri tuone, kwetu ni jicho tu huku tukifuatilia kinyemela nyemela watakapo kutana kwa mara ya 88 jumapili hii uwanjani Kasarani, Nairobi.