array(0) { } Radio Maisha | Nitawafunga Igwe wakati wa debi Jumapili - amesema Afriyie
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Nitawafunga Igwe wakati wa debi Jumapili - amesema Afriyie

Nitawafunga Igwe wakati wa debi Jumapili - amesema Afriyie

Mshambulizi wa Gormahia Francis Afriyie, ameionya AFC Leopards kwamba atawafunga Jumapili katika debi.

Akizungumza na idara ya michezo Redio Maisha mapema Jumamosi baada ya mazoezi mepesi, Afriyie alionesha uchangamfu.

“Kesho ni siku yetu wana Gormahia, lazima turudi kileleni. Kama mshambuliaji, hakuna utamu utakao linganishwa na ule wa kufunga mabao na kushinda mechi. Ni matumaini yangu hapo kesho tutashinda mechi hiyo dhidi ya AFC Leopards. Nikipewa nafasi, Nitajituma kadri ya uwezo wangu hadi nipate bao.” Alijipa moyo Afriyie.

Mshambulizi huyo kutoka Ghana mwenye umri wa miaka 24 alipata bao lake la kwanza akiichezea  Gormahia katika fainali ya ‘Super Cup’ dhidi ya Kariobangi Sharks.

“Niliingia mchezoni dakika za lala salama. Kwa ujumla nilikuwa na dakika saba pekee za kumwonesha kocha Pollack ya kwamba nina moyo wa Simba. Mechi kama zile zinahitajia ujasiri na uvumilivu. Kariobangi Sharks walionesha ubora wa kiufundi dakika zote tisini. Ni mechi ambayo kwamba wangetushinda iwapo hatungeimaliza mapema. Kufunga bao la pekee tena la ushindi chini ya dakika tatu baada ya kuingia mchezoni ni jambo ambalo limenipa motisha kubwa sana,” alisema Afriyie. Fainali hizo za Super Cup zilichezwa tarehe 20, Novemba kule Nakuru ugani Afraha.

Mahiri huyo mzaliwa wa Bong Ahafo kule Ghana, alianzia taaluma yake Bechem United. Baadaye aliondoka nyumbani kwao na kuelekea kule Serbia.

“ Babangu mzazi alitamani sana niichezee Asante Kotoko lakini sikupata nafasi. Kuna ushindani mkubwa sana Ghana haswa katika timu kubwa kama Kotoko. Lakini nilipata nafasi ya kujiunga na FK Vojvodina ya Serbia na baadaye Murcielagos Fc ya Mexico,” aliongezea Afriyie huku akikamilisha kwa kusema kwamba jumapili katika debi ni siku kubwa kwake na atakumbukwa na wakenya wazalendo wa Gormahia kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Afc leopards.

Afriyie alijiunga na Gormahia msimu huu akitokea Murcielagos Fc ya Mexico. Klabu hiyo ya Sinaloa ilikumbwa na misukosuko ya fedha baada ya wadhamini wakuu kujiondoa na ikabidi washushwe daraja.

Jumapili itashuhudia mechi ya watani ya 88 kati ya Gormahia na Afc leopards. Nchini Kenya pia udhamini wa mchezo wa kandanda kwa ujumla umekuwa kwa uchache, jambo ambalo kwa sasa Afriyie amesha zoea.

Sasa macho yote yataelekezwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani siku ya jumapili. Afriyie ambaye yuko katika hali nzuri kiafya, kisaikolojia na utimamu wa mwili kwa ujumla atakuwa anaitimiza ndoto yake iwapo ataifunga Afc leopards na Gormahia ipate ushindi. Kwetu sisi ni jicho tu, kila la heri Afriyie.