array(0) { } Radio Maisha | Ruto ampongeza Imran
Ruto ampongeza Imran

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Naibu wa Rais William Ruto amempongeza Imran Okoth, vilevile Mariga kwa kupata idadi kubwa ya kura zikilinganishwa na ilizopata Jubilee wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Ruto amesema licha ya vurugu na vitisho, idadi ya kura za Jubilee ziliongezeka zaidi ya mara dufu kutoka asilimia 12 hadi asilimia 26 ya kura zote zilizopigwa ikilinganishwa na Idadi ya ODM ambayo imepungua. Ruto amesema ODM ilipata asilimia 52 ya kura zote zilizopigwa kulinganisha na asilimia 78 ilizopata wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Viongozi wengine ambao wamempongeza Imran ni Gavana wa Kitui Charity Ngilu na Alfred Mutua wa Machakos waliokuwa wakimpigia debe Imran.