array(0) { } Radio Maisha | Vituo vya binafsi vya watahiniwa wa KCPE na KCSE kufutiliwa mbali

Vituo vya binafsi vya watahiniwa wa KCPE na KCSE kufutiliwa mbali

Vituo vya binafsi vya watahiniwa wa KCPE na KCSE kufutiliwa mbali

Na Sam Amani,

NAIROBI, KENYA, Huenda vituo vya binafsi vya watahiniwa wa Mitihani ya Kitaifa vikafutiliwa mbali kufikia mwaka ujao ikiwa miongoni mwa mikakati ya kukabili visa vya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa.

Hii ni baada ya watahiniwa binafsi katika Shule ya Msingi ya St Teresa Jijini Nairobi kukamatwa na kushtakiwa jana kwa kuhusishwa na udanganyifu katika mtihani wa kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema huenda maafisa waliokuwa wakilinda mtihani katika kituo hicho walilipwa ili wawasaidie watahiniwa hao kuiba mtihani.

Kulingana na Katibu katika Wizara ya Elimu Daktari Belio Kipsang vituo vya kibinafsi vinavyotumiwa kufanya mtihani vinaongoza katika visa vya majaribio ya kuiba mtihani. Aidha, amesema Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani Nchini KNEC zitajadiliana ili kuafikia mwafaka kuhusu namna ya watahiniwa hao watakavyokuwa wakifanya mtihani.

Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE ukiingia siku yake ya tano Ijumaa hii.