array(0) { } Radio Maisha | Wafuasi wa Mariga walaumiwa kufuatia ghasia Kibra

Wafuasi wa Mariga walaumiwa kufuatia ghasia Kibra

Wafuasi wa Mariga walaumiwa kufuatia ghasia Kibra

Na Mike Nyagwoka,

NAIROBI, KENYA, Wafuasi wa mgombea wa Chama cha Jubilee, McDonald Mariga wamelaumiwa pakubwa kufuatia ghasia ambazo zimeshuhudiwa mapema Alhamisi katika eneo la Kibra.

Kwa mujibu wa viongozi Chama cha ODM, vurugu zimeshuhudiwa pale kundi la vijana linalomuunga mkono Mariga walipofika Kibra na kuanza kuwahonga wapigakura.

Hata hivyo, viongozi wa Jubilee wakiongozwa na Mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa wamekana madai hayo wakisema ODM inawatumia vijana kuzua vurugu.

Mbunge huyo amewasihi polisi kuwachukulia hatua kali viongozi wa ODM kwa madai ya kuwachochea wakazi wa Kibra kuzua vurugu, hali ambayo amesema ni ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi.