array(0) { } Radio Maisha | Mchakato wa kumwondoa Gavana Waititu mamlakani wang'oa nanga

Mchakato wa kumwondoa Gavana Waititu mamlakani wang'oa nanga

Mchakato wa kumwondoa Gavana Waititu mamlakani wang'oa nanga

Na Omae Caren,

NAIROBI, KENYA, Masaibu yanaendelea kumwandama Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu huku mchakato wa kumwondoa mamlakanai ukianza rasmi.

Tayari wakazi wamewasilisha saini elfu mia mbili na kumi kwa bunge la kaunti. Wakiongozwa na viguvugu kwa jina Okoa Kiambu, wakazi hao wamelitaka bunge hilo la Kuanti kuharakisha shughuli ya kumwondoa gavana huyo wakidaia nahujumu utendakazi wa Kaunti.

Kiongozi wa Vuguvugu hilo Hoswell Kinuthia, amesema kwmaba kufuatia madai ya ufisadi yanayomkabili Waititu, hafai kuendelea kushikilia wadhfa wowote wa umma.

Hayo yanajiri huku Tume ya Uchaguzi IEBC, ikisema imekamiliha shughuli za kuzichunguza saini za wapigakura zilizowasilishwa mbele yake kufanikisha mchakato wa kuivunja serikali ya  Kaunti ya Taita Taveta.

IEBC imesema kuwa saini elfu ishirini na moja, mia nane sitini na moja miongoni mwa elfu thelathini na tisa, mia tatu zilizowasiliswa zimewiana na sajili ya wapigakura wa Kaunti ya Taita Taveta.

Kulingana na kipengele cha 123 cha Sheria za Serikali za Kaunti, yeyote anayetaka kuivunja serikali lazima aungwe mkono na asilimi 10 ya wapigakura wa kaunti inayohusika.

Ikumbukwe Kaunti ya Taita Taveta ina jumla ya wapigakura elfu mia moja hamsini na tano, mia saba kumi na sita kulingana na sajili ya mwaka 2017. Mwenyekiti wa IEBC,  Wafula Chebukati alipokea ombi kutoka kwa Gavana Grantom Samboja, Oktoba 31 kukagua saini hizo zilizokuwa zimewasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyattta.

Kuidhinishwa kwa saini hizo sasa kunatoa nafasi kwa Rais Kenyatta kubuni jopo maalum kumchunguza Gavana Samboja ili kubaini iwapo anastahili kuondolew mamlakani au la.