array(0) { } Radio Maisha | Watahiniwa 26 wa KCSE wahusishwa na udanganyifu

Watahiniwa 26 wa KCSE wahusishwa na udanganyifu

Watahiniwa 26 wa KCSE wahusishwa na udanganyifu

Na Sam Amani,

NAIROBI, KENYA, Huku mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nnne KCSE ukiendelea kote nchini, watahiniwa ishirini na sita waliokamatwa hapa jijini Nairobi wakihusishwa na undanganyifu wataendelea kuzuiliwa uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.

Afisa Mkuu wa Idara ya Upelelezi katika eneo la Starehe Martin Mbaya amesema uchunguzi unaendeshwa kubaini ni nani hasa aliyekuwa akiwatumia majibu ya mtihani wa Kemia karatasi la pili.

Watahaniwa hao walikamatwa katika Shule ya Msingi ya Wavulana ya St Teresa ambapo wanafunzi mia moja hamsini na wanne wa binafsi wanaoufanya mtihani wao.

Aidha maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI walifanikiwa kunasa simu thelathini na tano zinazoaminika kutumika kufanikisha udanganyifu katika mtihani huo. Tayari wamiliki wa simu ishirini na sita miongoni mwa thelathini na tano tayari wamejulikana na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

Kwingineko mjini Kisii jumla ya watahiniwa ishirini na sita waliokuwa wakifanyia mtihani wao katika Shule ya  binafsi ya Ramasha  hawakufika kuifanya mitihani yao siku moja tu baada ya watu kumi na mmoja kukamatw akatika shuel iyo hiyo wakihusishwa na udanganyifu. Miongoni mwa watahiniwa mia moja na watatu waliokuwa wamesajiliwa ni sabini pekee wanaoendelea na mtihani huo.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema kuwa washukiwa wengine kumi na wawili wanaendelea kuzuiliwa uchunguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.