array(0) { } Radio Maisha | Uchaguzi Mdogo wa Kibra wang'oa nanga

Uchaguzi Mdogo wa Kibra wang'oa nanga

Uchaguzi Mdogo wa Kibra wang'oa nanga

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura kikiwamo kile cha Shule ya Msingi ya Joseph Kang'ethe huku shughuli hiyo ikiendelea.

Aidha, kumeshuhudiwa mkanganyiko katika Kituo cha Kupiga kura cha Shule ya Msingi ya Kibra ambayo ina vituo viwili vya kupigia kura baada ya mpiga kuwa mmoja kukosa jina lake katika sajili ya wapiga kura.

Akizungumza katika Shule ya Msingi ya Kibra, Mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha Morden Alliance Party Martin Andati amesema kuhamishwa kwa vituo viwili hadi katika shule hiyo kimewachanganya baadhi ya wakazi ambao walikuwa wamerauka katika maeneo ya awali ya kupigia kura.

Inaarifiwa kuwa huenda mkanganyiko huo umechangiwa zaidi na kuhamishwa kwa baadhi ya vituo vya kupigia kura kufuatia mtihani wa kitaifa ya kidato cha nne inayoendelea.

Wakati uo huo, Mgombea wa Kiti hicho kwa Tiketi ya Chama cha ODM Imran Bernard Okth atapiga kura yake saa nne katika KAG OLympic, kabla ya kuandamana na Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga saa tano asubuhi katika Shule ya Msingi ya Old Kibra ambapo atapigia kura yake.

Vilevile, katika uchaguzi huu wagombea wa Jubilee Mackdonald Mariga na mwenziwe wa Ford Kenya hawatajipigia kura kwa kuwa si wapiga kura wa eneo hilo, licha ya kukiwania kiti hicho.

Naye mgombea huru Okoth Opondo akipiga akitarajiwa kupiga kura katika eneo la KAG Olympic mwendo wa saa nne huku Editor Ochieng wa Chama cha Ukweli Partu akipiga kura katika Shule ya Msingi ya Ayany.