array(0) { } Radio Maisha | Wakufunzi wa Nyumbani ni bora, tuwe na imani. Amesema Ambajo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakufunzi wa Nyumbani ni bora, tuwe na imani. Amesema Ambajo

Wakufunzi wa Nyumbani ni bora, tuwe na imani. Amesema Ambajo

Afisa mkuu mtendaji wa Klabu ya Sofapaka FC amewarai waajiri wa vilabu vya kandanda nchini wawe na imani na wakufunzi wa nyumbani kuliko wa kigeni.

Akizungumza na idara ya michezo Redio Maisha Jumatano mchana, Ambajo alisikitikia hali ya kandanda nchini.

“Kuna umuhimu mkubwa kwa vilabu vya hapa nchini Kenya kuwaamini wakufunzi wazawa. Wageni ni wazuri, wana tajriba na masomo ya hali ya juu lakini hawaelewi jinsi mambo huendeshwa barani Afrika. Haswa Kenya, lazima ujue utaratibu wa serikali, shirikisho la kandanda FKF na pia ligii kuu nchini KPL.Wageni hawatambui mambo haya,” Ambajo alinung’unika huku akiongezea pia ya kwamba wachezaji wakenya wana ukuruba mkubwa na wakufunzi wakenya wenzao kuliko wakufunzi wa kigeni.

Klabu ya Sofapaka FC msimu huu ilimwajiri mreno Divaldo Alves mwenye umri wa miaka 41, mzawa wa jiji la Luanda kule Angola. Mreno huyo ana leseni ya Euefa Pro, leseni ya juu zaidi kwa mujibu wa shirikisho la kandanda barani ulaya EUFA kimafunzo. Bila leseni hiyo ya mafunzo ya juu zaidi, huwezi funza klabu yeyote ambayo inashiriki ligii kuu katika taifa lolote barani ulaya.

“Ni kweli kwamba kuna umuhimu wa mkufunzi aliye na masomo ya juu sawia pia na wachezaji. Lakini kumbuka ya kwamba watu hawa ni ghali. Mkufunzi mgeni utamlipa mamilioni ya hela. Nchini Kenya kwa sasa hata ligii yenyewe haina udhamini, kwa hivyo hela za kumlipa huyu mkufunzi mgeni wataka zitoke wapi ilhali wachezaji wako bado hujawalipa” aliuliza Ambajo kwa ghadhabu.

Naibu mkufunzi wa Sofapaka fc John Baraza kwa sasa, msimu jana aliiwezesha klabu hiyo kumaliza nafasi ya tatu katika jedwali la ligii kuu nchini KPL. Ikumbukwe pia msimu juzi 2016/2017, aliitoa timu hiyo katika nafasi ya saba hadi kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Gormahia.

“Nina imani ya kwamba kama bado tungekuwa na Baraza usukani, huenda Gormahia msimu huu wangemaliza nyuma yetu. Lakini mambo bado, tusikate tamaa wanasofapaka maanake ndio tumeanza vibaya lakini tuna nafasi ya kujirekebisha na kurejea kileleni ipasavyo. Wachezaji wetu nafikiri bado wako katika ile hali ya kumzoea Divaldo Alves na filosofia yake.” alimalizia afisa huyo mkuu mtendaji wa Sofapaka fc.

Klabu ya Sofapaka kwa sasa iko katika nafasi ya 12. Baada ya kucheza mechi nane. Vijana hao wa ‘Batoto ba Mungu’ wana alama nane pekee.

Walikuwa mabingwa wa Ligii kuu nchini KPL mwaka wa 2009 wakati huo chini ya mkufunzi Robert Matano. Waliingia ligini kwa kishindo na fujo za hela ambazo zilisababishwa na mdhamini mkuu mwenye kiti bwanyenye mkongomani Elly Kalekwa.

Ikumbukwe pia huo ndio ulikuwa msimu wao wa kwanza kushiriki ligii kuu nchini. Kwa sasa wengi mashabiki wao wanasubiria ile siku ambayo kwamba Sofapaka itarudi tena kileleni. Swala bado lasalia kuwa ni je, hadi lini