array(0) { } Radio Maisha | Ombi lililowasilishwa kumwondoa Gavana Samboja Mamlakani linaafikia vigezo
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ombi lililowasilishwa kumwondoa Gavana Samboja Mamlakani linaafikia vigezo

Ombi lililowasilishwa kumwondoa Gavana Samboja Mamlakani linaafikia vigezo

Tume ya Uchaguzi IEBC, imetangaza kukamilisha shughuli za kuchunguza saini za wapigakura zilizowasilishwa mbele yake kufanikisha mchakato wa kuivunja Kaunti ya Taita Taveta. IEBC imesema kuwa saini  elfu ishirini na moja, mia nane sitini na moja miongoni mwa elfu thelathini na tisa, mia tatu zilizowasiliswa zimewiana na sajili ya wapiga kura wa Kaunti ya Taita Taveta.

Katika kipengele cha 123 cha Sheria za Serikali za Kaunti, yeyote anayetaka kuivunja serikali lazima aungwe mkono na asilimi 10 ya wapiga kura wa Kaunti husika.

Kufikia Machi mwaka wa 2017, Kaunti ya Taita Taveta ilikuwa na wapiga kura elfu mia moja hamsini na tano, mia saba kumi na sita .Mwenyekiti wa IEBC  Wafula Chebukati alipokea ombi kutoka kwa Gavana Grantom Samboja, Oktoba 31 kukagua saini hizo.

Gavana Samboja aliafikia uamuzi huo kufuatia mzozo baina yake na Wawakilishi wadi kuhusu bajeti ya mwaka wa kifedha 2019-2020, wawakilishi wakimlaumu kwa kutakaa kupitisha makadirio ya bajeti hiyo.

Samboja aidha alipata afueni baada ya baada ya seneti kufutilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa dhidi yake na wawakilishi waliokuwa wamepotisha hoja ya kumbandua mamlakani.

Kamati Maalum ya Seneti iliyobuniwa kuchunguza malalamiko hayo ilisema sababu zilizotolewa na viongozi hao hazitoshi kumng'oa madarakani.