array(0) { } Radio Maisha | Walinzi 4 wa Sonko wakamatwa tena punde baada ya kuachiliwa

Walinzi 4 wa Sonko wakamatwa tena punde baada ya kuachiliwa

Walinzi 4 wa Sonko wakamatwa tena punde baada ya kuachiliwa

Walinzi wanne wa Gavana wa Nairobi Mike Sonko walioachiliwa kwa thamana ya shilingi laki moja baada ya kukamatwa Jumatatu kufuatia mvutano baina ya polisi na Gavana Mike Sonko wamekamatwa tena.

John Abok, Joseph Mwangi Karai, Kennedy Odhiambo na Richard Bosire walikamatwa punde baada ya kuondoka korokoroni.

Wanne hao walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani Kennedy Cheruyot ambapo walikana mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili.

Inadaiwa washukiwa walipinga kukamatwa kwao. Katika mahakama nyingine washukiwa ao hao wanakabiliwa na mashtaka ya kufanya mkutano haramu nje ya Makao Makuu ya Idara ya Upelelezi DCI.

Ikumbukwe makabiliano makali yalishuhudiwa nje ya EACC baina ya polisi na wafuasi wa Sonko alipofika kurekopdi taarifa kufuatia madai ya kutoa taarifa za uongo mwaka 2017 wakati alipokuwa akitafuta idhini ya kuwania wadhfa wa Ugavana. EACC inamshtumu Sonko kuwa hafai kushikilia wadhfa huo kwani alishawahi kuhukumiwa mwaka 1997.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba tarehe 20.