array(0) { } Radio Maisha | Watu 10 wakiwamo polisi 2 wameuliwa Jaldesa, Marsabit

Watu 10 wakiwamo polisi 2 wameuliwa Jaldesa, Marsabit

Watu 10 wakiwamo polisi 2 wameuliwa Jaldesa, Marsabit

Watu kumi wakiwamo maafisa wawili wa polisi wameuliwa kufuatia uvamizi kwenye eneo la Jaldesa,  Kaunti ya Marsabit. Kwa sasa maafisa wa usalama wanafanya mkutano wa dharura, huku usalama ukiwa umeimarishwa..

Inaarifiwa kwamba wavamizi walilivamia gari kisha kuwaua watu watatu huku wengine saba wakifariki dunia kufuatia makabiliano baiana ya wenyeji na wavamizi hao.