array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Kaskazini Mashariki wapinga ripoti ya sensa

Viongozi wa Kaskazini Mashariki wapinga ripoti ya sensa

Viongozi wa Kaskazini Mashariki wapinga ripoti ya sensa

Viongozi wa eneo la Kaskazini Mashariki ya nchi, wamepinga matokeo ya sensa ya mwaka wa 2019 wakisema kuwa takwimu zilizotolewa zimekumbwa na dosari wakipendekeza shughuli hiyo kurejelewa mara moja.

Takribani viongozi ishirini na watano wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Aden Duale, wamepuuza matokea hayo wakisema kwamba, data zilizotumika kutoa matokeo hayo zimetolewa kutoka kwa shughuli ya majaribio yaliofanywa kabla ya sensa ya mwaka huu.

Duale aidha amesema kuwa matokeo ya hivi maajuzi yanaonesha kuwa hapakuwapo na ongezeko la watu kwenye Kaunti za Mashariki ya nchi, hatua inayokinzana na mwongozo kuhusu ukuaji wa watu na takwimu za majribio ya Shirika la Kitaifa la Takwimu KNBS.

Viongozi hao sasa wanashinikiza kufutiliwa mbali kwa matokeo hayo wakisema kwamba, itahujumu shughuli za kutolewa kwa mgao wa fedha kwa kaunti za eneo hilo , hasa baada ya idadi kubwa ya watoto kuongezeka baada ya sensa ya miaka nyuma.