array(0) { } Radio Maisha | Uwanja wa city stadium kupewa sura mpya
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Uwanja wa city stadium kupewa sura mpya

Uwanja wa city stadium kupewa sura mpya

Uga wa jiji la Nairobi maarufu ‘Nairobi City Stadium’ utapewa sura mpya hivi karibuni, amesema Mwenyekiti wa Bodi Teule ya Michezo katika Kaunti ya Nairobi  Hashim Kamau.

Akizungumza na idara ya michezo Redio Maisha, Kamau amewapa matumaini wanamichezo na wakaazi wa Nairobi kwamba hatua hiyo itafanikisha shughuli za michezo na kuinua vipaji vya vijana.


Kamau aidha amesema shughuli za ukarabati zimeshaanza akiwataka namichezo kuwa na subira  uwanja huo wa kihistoria ukipewa  sura mpya. Kamau  ameongeza  kwamba zulia jipya lishafika na linangojea mhandisi tu kulitandaza uwanjani lakini hakuwa na uhakika wa muda halisi wa uwanja huo kukamilika.


Ni miaka takriban kumi na mitano sasa tangu uwanja huo wa Nairobi City Stadium ushughulikiwe. Shirikisho la Kandanda nchini FKF mwaka wa 2008, wakati huo kamati teule ikiongozwa na Titus Kasuve na Mohammed Hatimy iliweza kupata mgao wa shilingi milioni 25 kutoka kwa shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA  kukarabati uwanja huo.


Chini ya mradi wa ‘Win in Africa for Africa’, kuongezea kwa hela hizo, uwanja huo ulipata zulia jipya ambalo pia FIFA ilitoa kwa Wakenya bure bwerere. Wahandisi na wataalam ambao walitandaza  zulia hilo pia waligharamiwa na FIFA katika kile kimetajwa kuwa uzalendo


 Mechi za ligii kuu nchini KPL zilichezwa hapa na kusababisha ligii ya humu nchini ikiboreka sana kwa sababu mazingira mazuri.

Uwanja huo sasa utagharamiwa na Kaunti ya Nairobi na kulingana na mhandisi mkuu, unatarajia uwe na uwezo wa kuwadhibiti takriban mashabiki elfu 20. Pia ukiwa na sehemu maalum ya biashara ambayo itakuwa na mikahawa na maduka. Wanariadha wakimbiaji pia watapata afueni kwa sababu mipango ipo ya kutandaza zulia la kukimbilia.


Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Dakta Evans Idero na waziri wa michezo katika kaunti ya Nairobi wakati huo bi Ann Lokidor walikuwa na mpango wa kukarabati uwanja wa city. Tetesi zasema kwamba tayari shilingi milioni 100 zilitengwa kando kushughulikia mradi huo ambao haukutekelezwa

Japo bwana Hashim Kamau hajatoa kitita taslim cha pesa ambazo zimetengewa mradi huo, lakini ni afueni kubwa kwa wakaazi wa Nairobi.

Uwanja wa Nairobi City Stadium umetumika pakubwa kama uwanja wa mechi za nyumbani kwa vigogo Gormahia. Mashabiki wa K’ogalo basi hawatakuwa na budi ila kusema afadhali leo kuliko jana iwapo watarudi katika uwanja huo na waupate ukiwa katika hali ya kung’aa mwaka ujao.