array(0) { } Radio Maisha | Wabunge washindwa kubadilisha kipengele cha kuthibiti viwango vya riba kutokana na idadi

Wabunge washindwa kubadilisha kipengele cha kuthibiti viwango vya riba kutokana na idadi

Wabunge washindwa kubadilisha kipengele cha kuthibiti viwango vya riba kutokana na idadi

Wakenya wataendelea kupata mikopo kutoka kwa benki mbalimbali nchini kwa viwango vya riba vitakavyowekwa na benki hizo baada ya wabunge kukosa kufikia idadi inayohitajika ili kubadilisha kiwango cha riba cha asilimia kumi na nne kilichowekwa awali.

Ni hatua ambayo imeilazimu bunge hilo aidha kusitisha vikao vyake baada ya wabunge kutosa kuafikia idadi kamili kuwaruhusu kubadilisha viwango vya riba.

Takribani wabunge mia mbili thelathini na watatu walihitajika kupiga kura baada ya wabunge mia moja sitini na mmoja kufika bungeni.

Hatua hii inamaanisha kuwa benki zinauwezo wa kubadilisha kiwango cha riba inachotaka kwa wanaochukua mikopo kuambatana na kipengele cha thelathini na tatu (B).