array(0) { } Radio Maisha | Viongozi wa Tharaka Nithi wametishia kuwasilisha kesi kupinga matokeo ya sensa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Viongozi wa Tharaka Nithi wametishia kuwasilisha kesi kupinga matokeo ya sensa

Viongozi wa Tharaka Nithi wametishia kuwasilisha kesi kupinga matokeo ya sensa

Siku moja tu baada ya Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu, KNBS kutoa ripoti ya sensa mwaka wa 2019, baadhi ya viongozi wa Kaunti ya Tharaka Nithi wametishia kuwasilisha kesi mahakamani kuyapinga matokeo hayo.

Gavana wa kaunti hiyo Muthomi Njuki amesema idadi ya watu wa Tharaka Nithi si watu elfu mia tatu tisini na tatu, mia moja sabini na saba jinsi inavyodaiwa na KNBS. Njuki ameitaka KNBS kurejelea shughuli hiyo katika eneo lake akisema idadi hiyo si kweli.

Wakati uo huo, Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amesema ni sharti KNBS itoe maelezo ni kwa nini Meru ilirekodi idadi ndogo ya watu. Amesema idadi ya watu milioni 1.6 ni ya chini mno na hivyo taasisi hiyo inawahadaa wakazi wa kaunti hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Maara, Mbiuki Kareke amesema eneo hilo limekuwa likitumiwa na viongozi kujipatia kura ilhali wakati huu wa sensa wanabaguliwa. Amesema haiwezekani kwa wao kuridhia matokeo haya hasa ikizingatiwa idadi ya kura ambazo zimekuwa zikipigwa Tharaka Nithi.

Hata hivyo, Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga amewashauri viongozi hao kukoma kuibua maswali kuhusu matokeo ya sensa ilhali hawakuendesha shughuli hiyo. Kahiga amesema maafisa wa KNBS ni watu wenye tajriba ya juu na kamwe hawangeweza kutoa matokeo kinyume na matarajio yao. Gavana huyo aidha amesema idadi ya watu wa Nyeri ni sawa licha ya malalamishi ya baadhi ya viongozi.

Kaunti ya Nyeri ina watu watu elfu mia saba hamsini na tisa, mia moja sitini nane. Kwa mujibu wa KNBS idadi ya watu nchini ni milioni 47.6, idadi hii ikiongezeka kutoka watu milioni 37.7 wakati wa sensa ya mwaka wa 2009.