array(0) { } Radio Maisha | Wakenya milioni 8.1 bado wanatumia kuni kupikia

Wakenya milioni 8.1 bado wanatumia kuni kupikia

Wakenya milioni 8.1 bado wanatumia kuni kupikia

Huku Mashirika ya Kimataifa yakiendelea kuweka mikakati ya kuboresha mbinu za mapishi ikiwa njia ya kuboresha mazingira na afya, imebainika kuwa Wakenya milioni 8.1 ambao ni asilimia 64.7 wanatumia kuni kupikia ,asilimia 19 ambao ni milioni 2.4 wakitumia gesi na asilimia 10 ambao ni Wakenya milioni 1.3 wakitumia makaa.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo ya upishi wa kisasa bila kutumia vifaa vya kudhuru afya ya binadamu Clean Cooking Forum  jijini Nairobi, Waziri wa Kawi, Charles Keter amesema kwamba wizara yake itahakikisha kuwa kufikia mwaka 2030, asilimia kubwa ya Wakenya wanapika bila kudhuru afya wala kuharibu mazingira.

Ripoti hiyo imeonyesha kwamba vifaa hivyo vya kudhuru afya vimesabaisha vifo zaidi ya elfu 21 kila mwaka. Vilevile idadi ya nyumba zinazopikia kuni imeongezeka kutoka milioni 4.7 hadi milioni 7.3 kwa muda wa miongo miwili iliyopita.

Nyumba milioni 5.5 zinamiliki jiko la makaa, nyumba milioni 1.7 zinatumia mafuta ya taa kupikia huku idadi ya wanaotumia gesi ikiongezeka mara sita kutoka elfu mia sita hadi milioni 3.7 kwa muda wa miongo miwili. Vilevile asilimia 54 ya wanaotumia gesi wako mijini huku asilimia 18 wakiwa mashinani.

Ni asilimia 3 pekee ya wanaotumia umeme kupikia.

Katibu wa Wizara ya Mazingira, Betty Maina kwa upande amesisitiza kuwa wanaoathirika zaidi ni akina mama na watoto walio katika mitaa ya mabanda, hivyo mikakati ya kuboresha mapishi ikiwekwa ni sharti wazingatie bei.