array(0) { } Radio Maisha | Katibu wa COTU Francis Atwoli amemtetea Jaji Mkuu kuhusu mgao wa fedha
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Katibu wa COTU Francis Atwoli amemtetea Jaji Mkuu kuhusu mgao wa fedha

Katibu wa COTU Francis Atwoli amemtetea Jaji Mkuu kuhusu mgao wa fedha

Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi, COTU Francis Atwoli amemtetea Jaji Mkuu David Maraga akisema kuwa idara ya mahakama inastahili kutengewa fedha za kutosha ili kuendeshea shughuli zake.

Wakati wa kikao na wanahabari, Atwoli aidha amemshauri Rais Uhuru Kenyatta kuangazia upya mgao wa fedha zilizotengewa Idara ya Mahakama akisisitiza haja ya idara hiyo kuwa kipaumbele ili kukabili vita dhidi ya ufisadi.

Amesema iwapo idara hiyo itatengewa fedha za kutosha basi kesi za ufisadi zitasikilizwa na kuamuliwa kwa wakati ufaao. Kwa mujibu wa Atwoli, taifa la Kenya ambalo wananchi wake wameendelea kufurahia demokrasia linapaswa kuzipa uhuru idara mbalimbali kutekeleza majukumu yake kikamilifu bila kuingiliwa na idara nyingine za serikali.

Atwoli aidha ameionya serikali dhidi ya kuingiza siasa suala hilo akisema huenda ikawatatiza mamilioni ya Wakenya kupata haki.

Kauli ya Atwoli inajiri siku moja tu baada ya Jaji Mkuu David Maraga kulalamikia hatua ya serikali kuupunguza mgao wa fedha unaotengewa idara hiyo akisema tayari shughuli mbalimbali katika Idara ya Mahakama zimeathirika katika maeneo mbalimbali nchini