array(0) { } Radio Maisha | Watu kumi na mmoja wamenaswa Kisii wakijifanya watahiniwa wa KCSE
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Watu kumi na mmoja wamenaswa Kisii wakijifanya watahiniwa wa KCSE

Watu kumi na mmoja wamenaswa Kisii wakijifanya watahiniwa wa KCSE

Maafisa wa polisi katika Kituo cha Kisii ya Kati kwenye Kaunti ya Kisii wamewatia mbaroni watu kumi na mmoja kwa kujifanya watahiniwa wa Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne, KCSE.

Inaarifiwa maafisa wa elimu pamoja na polisi wamevamia Shule ya Binafsi ya Ramasha ambapo wamefanikiwa kuwanasa kumi na mmoja hao. Aidha, idadi isiyojulikana ya washukiwa wamefanikiwa kutoroka.

 

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ametoroka ila polisi wamefanikiwa kumkamata Naibu wake ambaye tayari alikuwa amezichukua karatasi za KCSE katika kituo hicho.

Kamanda wa Polisi wa Kisii ya Kati, Zachary Kimani na afisa wa idara ya upelelezi eneo hilo, Martin Korongo wamesema maafisa wa elimu vilevile wataadhibiwa kufuatia utepetevu.