array(0) { } Radio Maisha | Rais Kenyatta amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kibiashara
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Kenyatta amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kibiashara

Rais Kenyatta amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kibiashara

Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ili kuendelea kuimarisha uchumi wa taifa, amesema Rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Walipa Kodi inayoendelea hapa jijini Nairobi, Rais amesema kuwa mlipakodi amechangia pakubwa katika ustawi wa uchumi wa taifa hili.

Kenyatta amesema serikali yake itaendelea kuweka sera zitakazotoa mazingira bora kwa wawekezaji wa binafsi kuwekeza nchini ili kutoa nafasi za ajira kwa mamia ya vijana wanaofuzu katika taasisi mbalimbali kando na kuchangia katika uchumi wa taifa.

Kuhusu suala la wanaokwepa kulipa kodi, Rais Kenyatta ameitaka Idara ya Mahakama kutekeleza jukumu lake bila uoga wowote ili kuhakikisha kuwa wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria. Katika kikao hicho aidha Kenyatta ameitania idara hiyo kufuatia mvutano unaoendelea kuhusu mgao wa fedha kwenye idara ya mahakama.

Wakati uo huo, Rais Kenyatta ameunga mkono juhudi za Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Umma za kusuluhisha kesi kwa nje ya mahakama yaani Plea Bargaining, huku akiziagiza Idara ya Upelelezi DCI na Ofisi ya Mkuu Mashtaka kuwakamata watakaokiuka sheria ya kulipa kodi.