array(0) { } Radio Maisha | Gavana Mike Sonko ahojiwa na EACC kuhusu taarifa za kupotosha
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Gavana Mike Sonko ahojiwa na EACC kuhusu taarifa za kupotosha

Gavana Mike Sonko ahojiwa na EACC kuhusu taarifa za kupotosha

 

Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema kamwe hatatishwa na wale wanaolenga kumdhalilisha na kumzuia kutekeleza maendeleo kwa manufaa ya wakazi wa Nairobi. Sonko aidha amedai kuwa analengwa katika vita dhidi ya ufisadi na mahasimu wake.

Sonko mapema leo amefika katika Makao Makuu ya Tume ya Maadili na Kuukabili  Ufisadi EACC, kuhojiwa akiandamana na wafwasi wake ambao wamekabiwa kwa vitoza machoza na Polisi wa kukabili ghasia.

Shughuli za kibiashara na uchukuzi katika barabara zilizoko karibu na Jumba la Integrity zilitatizika kwa muda baada ya polisi kuwafurusha wafuasi hao kwa kuwarushia vitoza-machozi. Aidha waandishi wa habari hawakuzwa huku Sonko akiwazuia kuingia katika jumba hilo.

Sonko amehojiwa kuhusu madai ya kutoa taarifa za kupotosha alipowania ugavana mwaka 2017 huku akiilaumu EACC kwa madai ya kumlenga pasi na kuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake.

Gavana Sonko vilevile amesema kuwa analengwa na wanaotaka kumuondoa katika siasa za Nairobi akisema kuwa hatatishika.

Kwa upande wake Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owimo ameisuta serikali kwa mada ia kumlenga Sonko isivyostahili akisema kuwa hali hiyo itaathiri maendeleo ya Nairobi.

Hayo yanajiri huku Mahakama ya Nairobi, ikiagiza kuendelea kuzuiliwa kwa siku tano mtu mmoja ambaye amekuwa akiwalaghai wakazi wa Nairobi akijifanya kuwa Gavana Mike Sonko.

Mshukiwa Geoffrey Mandela anadaiwa kutumia akaunti mbalimbali kwa jina la Sonko na kuwalaghai wakazi.

Hakimu wa Mahakama ya Milimani Martha Nanzushi ameridhia ombi la Upande wa Mashtaka kuendelea kuzuiliwa kwa mshukiwa ili kukamilisha uchunguzi dhidi yake.

Afisa wa Upelelezi Urbanus Munguti, ameiambia mahakama kuwa uchunguzi huo unaohusisha ulaghai kutumia stakabadhi bandia za Kaunti ya Nairobi na kwamba unahitaji muda zaidi.