array(0) { } Radio Maisha | Wakuu wa tano wa polisi wahamishwa

Wakuu wa tano wa polisi wahamishwa

Wakuu wa tano wa polisi wahamishwa

Maafisa watano wakuu wa polisi, akiwamo Kamanda wa Chuo cha Mafunzi ya Polisi King'ori Mwangi na aliyekuwa Mkuu wa Kitengi cha GSU, William Sayia wamehamishwa hadi Tume ya Huduma za Umma.

Kwa mujibu wa mabadiliko ya hivi karibuni katika Idara ya Polisi, muhula wa kuhudumu wa Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi - Edward Mbugua kwa kipindi cha miaka minne, wadhifa ambao umekuwa ukimezewa mate kwa muda sasa.

Maafisa wengine waliohamishwa ni; Stanely Cheruiyot ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Uanasheria katika Idara ya Polisi, Kitoo Kapchanga na Peter Mwania aliyekuwa akihudumu katika Makao Makuu ya Idara hiyo.