array(0) { } Radio Maisha | Polisi wa Kitui wanalisaka kundi la vijana waliombaka ajuza kwa zamu

Polisi wa Kitui wanalisaka kundi la vijana waliombaka ajuza kwa zamu

Polisi wa Kitui wanalisaka kundi la vijana waliombaka ajuza kwa zamu

Polisi kwenye eneo kaunti Ndogo ya Lower Yatta, Kaunti ya Kitui wameimarisha msako dhidi ya kundi la vijana waliovamia makazi ya ajuza mmoja na kumbaka kwa zamu.

Kamanda wa Polisi eneo hilo Charles Chacha amesema kwamba licha ya kitendo hicho kufanyika Jumamosi usiku, kiliripotiwa Jumapili jioni. Aidha, Chache amesema kwamba kufikia jana jioni, walikuwa hawajapokea ripoti kamili ya matibabu

Uchunguzi wa awali umebainisha kwamba ajuza huyo mwenye umri wa miaka 102, alivamiwa nyumbani kwake kabla ya kucharazwa na kisha kubakwa na wanaume ambao kufikia sasa idadi yao haijulikani.

Kisa hiki kinajiri wakati Kamishna wa Kaunti ya Kitui Boaz Cherutich akidokeza kwamba kaunti hiyo inaoongoza kwa idadi ya visa vya ubakaji na unajisi ikilinganishwa na kaunti zingine eneo la Mashariki.