array(0) { } Radio Maisha | TSC imeanzisha mchakato wa kuvunja mkataba na Chama cha KNUT
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

TSC imeanzisha mchakato wa kuvunja mkataba na Chama cha KNUT

TSC imeanzisha mchakato wa kuvunja mkataba na Chama cha KNUT

Wiki moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT, Wilson Sossion kuondolewa kwenye sajili ya walimu mambo yanazidi kuchacha kwa chama hicho baada ya Tume ya Huduma za Walimu TSC sasa kuanza mchakato wa kuvunja uhusiano na chama hicho.

Tume ya Huduma za Walimu TSC, imetoa notisi ya miezi miwili kabla ya kuvunja mkataba wa miaka 51 baina yake na Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT ambacho kimedumu kwa takriban miaka 60.

Katika barua iliyoandikwa Novemba 4, Afisa Mkuu Mtendaji wa wa TSC Nancy Macharia, amesema kuwa mkataba huo uliotiwa saini miaka 51 iliyopita utavunjwa kwa misingi kwamba idadi ya wanachama wa KNUT kwa sasa imepungua na kuwa chini ya asilimia 50 ya walimu wote waliosajiliwa nchini na hivyo kwa mujibu wa Sheria za Leba chama hicho hakitoshi kutambulika kuwa chama cha kitaifa cha kuwawakilisha walimu.

Kwa mujibu wa takwimu za TSC, kuna walimu lfu 318 huku waliosajiliw ana KNUT wakiwa elfu 115 pekee. Ili kuafikia idadi hiyo KNUT inahutaji walimu 159. Idadi kubwa ya walimu wamejiondoa baada ya TSC kukataa kuwaongeza mshahara walio kwenye KNUT kufuatia uamuzi wa mahakama mapema mwaka huu

Iwapo mkataba huo utavunjwa basi KNUT, mamlaka ya KNUT  kuendesha shughuli zozote kwa niaba ya walimu  yatapungua na kuendeleza vita vikali ambavyo vimeshuhidiwa dhidi ya KNUT na hasa katibu wake mkuu Wilson Sossion. Kwa wakati mmoja Wilson Sossion aliondolewa kwenye uongozi na Baraza la Kitaifa lakini uamuzi wa mahakama ukamrejesha. Kadhalika mahakama vilevile iliamua kwamba anaweza kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa KNUT hata baada ya kuondolewa katiak sajili ya wapiga kura.