array(0) { } Radio Maisha | Rais Uhuru Kenyatta ashtumiwa vikali
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Rais Uhuru Kenyatta ashtumiwa vikali

Rais Uhuru Kenyatta ashtumiwa vikali

Rais Uhuru Kenyatta ameshtumiwa vikali kwa madai kwamba serikali yake imeendelea kukiuka katiba. Mmoja wa wataalam walioiandika katiba ya sasa Pofesa Yash Pal Ghai, amesema hatua ya viongozi kuipuuza katiba hiyo imesababisha mivutano ya mara kwa mara inayoweza kusuluhishwa kwa kufuata sheria.

Ghai pamoja na watetezi wengine wa haki za binadamu akiwamo mwanauchumi David Ndii walizuiwa kuwahutubia wanachama wa Vuguvugu la Okoa Mombasa licha ya mwaliko baada ya mkutano huo kusitishwa.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wahubiri wa Dini ya Kiislamu wa Kutetea Haki za Binadamu MUHURI, Khelef Khalifa amesema watawasilisha kesi mahakamani kutafuta fidia baada ya kuzuiwa kufanya mkutano huo.

Wamesema walikuwa wameandaa mkutano huo na kulipia shilingi elfu ishirini na tano lakini wakaarifiwa baadaye na usimamizi wa Chuo Kikuu cha Technical Mjini Mombasa ambapo mkutano huo ulikuwa ufanyike kuwa umesitishwa.

Amesema walikuwa wametumia pesa nyingi kwa maandalizi na hawatakubali kuendelea kunyanyaswa

Ikumbukwe mvutano umekuwapo baina ya Vuguvugu hilo na serikali kufuatia usafirishaji wa makasha kutoka Mombasa hadi jijini Nairobi kupitia SGR.

 

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari , Simon Sang amesema hawapingi shughuli zote za SGR ila wanatafuta mazungumzo na serikali kuhusu utaratibu utakaotumika bila kuathiri uchumi wa eneo la Pwani.