array(0) { } Radio Maisha | Imran apuuza madai kwamba anamili akunti ya @Imran Twitter

Imran apuuza madai kwamba anamili akunti ya @Imran Twitter

Imran apuuza madai kwamba anamili akunti ya @Imran Twitter

Mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo la Kibra kupitia Chama cha ODM, Imran Bernard Okoth amepuuza madai kwamba anaimiliki akaunti ya mtandao wa Twitter inayodaiwa kuchapisha ujumbe kwamba mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Jubilee, McDonald Mariga ni mwizi wa sera zake miongoni mwa madai mengine.

Imran kupitia taarifa kwa vyombo vya habari amesema anafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba anayeeneza uvumi huo kupitia akaunti kwa jina @Imran_Okoth anakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Amewaonya wafuasi wake dhidi ya kuziamini jumbe zinazochapishwa kupitia akaunti hiyo, akisema anafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa akaunti yake rasmi inatambuliwa ili kuepuka mkanganyiko huo.

Wakati uo huo, amewashauri wafuasi wake kujitokeza kwa wingi tarehe saba mwezi huu ili kumchagua kuwa mbunge wao.

Imran ni miongoni mwa wagombea ishirini na wanne wanaotazamia kuchaguliwa, huku ushindani mkuu ukiwa baina yake na Mariga wa Jubilee.

Wengine ni Eliud Owalo wa ANC na Khamisi Butichi wa Ford Kenya miongoni mwa wengine