array(0) { } Radio Maisha | Muhiddin awataka wakenya kuwa na subra na FKF
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Muhiddin awataka wakenya kuwa na subra na FKF

Muhiddin awataka wakenya kuwa na subra na FKF

Aliyekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars  Twahir Muhiddin amewaomba Wakenya kuwa na subra na Shirikisho la Kandanda Nchini FKF.

Akizungumza na Meza ya Michezo ya Radio Maisha  wakati wa sherehe za mahafili ya ukufunzi wa raundi ya pili ya leseni za CAF C jijini  Nairobi, Ijumaa tarehe Mosi, Novemba, Muhddin alisisitiza haya,

“ Ukufunzi nchini Kenya ni jambo ambalo kwa sasa itabidi tulitilie maanani. Kandanda nchini itaboreka iwapo wakufunzi wetu wataonesha ubora wao''.

Mchezo huu umebadilika kwa sasa na wakufunzi wenye mafunzo ya hali ya  juu ndio bora. Leo hii nimefurahishwa sana na wakufunzi hawa ambao wamepata leseni ya CAF C,” alisema Muhddin akiwa katika taasisi ya Goan, jijini Nairobi.

Aidha amewarai Wakenya kuwa na subra huku akiiomba serikali kuongeza mchango wao katika sekta tofauti tofauti za michezo nchini.

“Lazima tuwekeze kwa michezo. Ni jukumu letu sote kama wakenya kuwa wazalendo na ikiwa basi hutajukumika basi wewe si mzalendo''.

''Nasikitika sana kuona Ligi Kuu Nchini KPL ikiwa katika hali duni ilhali Wakenya tunalipa ushuru,” alisikitika Muhdin ,huku akiongeza kwamba iwapo basi serikali itaipiga jeki FKF,  ifikapo mwaka wa 2020 azimio lao la kuwafunza wakufunzi elfu kumi kote nchini litatimia.

Muhddin kwa sasa ndiye Mkurugenzi wa Ufundi katika Timu ya Bandari fc na pia mwalimu wa masomo ya kandanda nchini chini ya Shirikisho la Kandanda Barani Afrika Caf.

Aliifunza Timu ya Taifa Hambee Stars mwaka wa 1990 Kombe la Bara Afrika,  Algeria.

“Chanda chema huvikwa pete. Kazi ambayo tuliifanya kule Algeria 1990 ilikubalika na uzalendo wetu ulionekana, kwa hivyo basi tuendelee hivyo hivyo bila kurudi nyuma''.

Lakini Wakenya lazima wawe watu wenye subra. Ona Wajerumani kwa mfano, iliwachukua takriban miaka kumi na minne kutengeza kikosi ambacho kilitwaa ubingwa wa dunia mwaka wa 2014, Brazil.

Wakenya tuwe na subra, kandanda nchini itaboreka. Tukumbuke pia tusiwe watu wa fitina, tujengane sote kwa pamoja.” Aliwahimiza Wakenya huku akiwaomba wawache siasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kozi hizo za leseni ya Caf C raundi za kwanza mwaka huu, zilianza Septemba tarehe mbili na kumalizika Octoba tarehe nne jijini Nairobi, Thika, Nakuru na Eldoret.

Walimu Wakuu ambao wameidhinishwa na CAF kuongoza hafla hizo walikuwa Twahir Muhddin, Leonard Saleh na George Ondula. Shughuli hii imewanufaisha mahafili tisini ambao kwa sasa wana leseni za Caf C.

Raundi ya pili nayo ilianza Octoba tarehe saba na kumalizika Novemba tarehe moja. Mafunzo haya yalifanyika na kumalizika jijini Nairobi katika taasisi ya Goan, jijini Kisumu yalikuwa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki na Machakos mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa kaunti hiyo mjini. Mahafili 180 walipata nafasi ya kufuzu na mafunzo ya Caf leseni C.

Muhddin kwa sasa analenga kueneza ukufunzi wa mchezo wa kandanda  kote nchini,  Ametaja maeneo ambayo yametengwa kimaendeleo na kuyasifia kuwa na mchango mkubwa sana katika mchezo wa kandanda .

Huko ndiko anako nuia kutua