array(0) { } Radio Maisha | Mshindi wa Saka Chapaa apatikana katika eneo la Pipeline, Nairobi
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mshindi wa Saka Chapaa apatikana katika eneo la Pipeline, Nairobi

Mshindi wa Saka Chapaa apatikana katika eneo la Pipeline, Nairobi

Hatimaye mshindi wa shindano la Saka Chapaa mtaani Pipeline, Nairobi amepatikana. Geoffrey Mutunga, mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na minane, ametangazwa mshindi baada ya kupata bahasha ya ushindi, katika shindalo hilo lililoanza mtaani humo Jumatatu wiki hii na kumalizika leo hii.

Wiki iliyopita, shindano la Saka Chapaa lilifanyika katika Mtaa wa Githurai 45 ambapo Julius Ndubiri Munene alijishindia shilingi elfu 50. Wiki iliyotangulia, Derick Wanjala mkazi wa Gatina, Kawangware, aliibuka mshindi. Shindano hili la Saka Chapaa limeingia wiki ya tatu jijini Nairobi.

Ili kutangazwa mshindi, unachohitajika kufanya ni kusaka bahasha yenye nembo ya Radio Maisha ya rangi ya majano na nyekundu, yenye saini ya Mkuu wa Redio Tom Japanni, ambayo hufichwa kwenye eneo ambalo shindano linafanyikia.

Kumbuka shilingi laki tatu zimetengwa kwa ajili ya washindi kwenye mitaa mbalimbali ya Nairobi, ambapo kila wiki, shilingi elfu 50 zitatolewa kwa anayepata bahasha ya ushindi.

Lengo la shindano la Saka Chapaa ni kuwazawidi mashabiki wa Radio Maisha, vilevile kuwapa fursa ya kutangamana na watangazaji wa kituo hiki namba moja kote nchini.