array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa mauji ya Monica Kimani, Joseph Irungui (Jowi) sharti aachiliwe, amesema Babu Owino
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mshukiwa wa mauji ya Monica Kimani, Joseph Irungui (Jowi) sharti aachiliwe, amesema Babu Owino

Mshukiwa wa mauji ya Monica Kimani, Joseph Irungui (Jowi) sharti aachiliwe, amesema Babu Owino

Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino sasa anashinikiza kuachiliwa kwa mshukiwa wa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, Joseph Irungu maarufu Jowi. Babu amesema ni dhuluma kwa Jowi kuendelea kuzuiliwa kwa muda mrefu bila ya kupewa dhamana.

Katika mtandao wake wa Facebook, Babu amesema Jowi lazima aachiliwe kwa dhamana au bondi kisha iwapo atapatikana na hatia ahukumiwe pasi na kuendelea kudhulumiwa.

Mbunge huyo ametilia shaka kwa nini mshukiwa huyo hajatendewa haki kufikia sasa huku akishuku huenda ni kwa sababu hana ushawishi akilinganishwa na wengine ambao wanakabiliwa na kesi za mauaji.

Jowi alinaswa Septemba mwaka uliopita akihusishwa na mauji ya Kimani na kuzuiliwa katika Gereza la Kamiti baada ya kukana mashtaka dhidi yake.

Mshukiwa huyo amejaribu mara mbili kuwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana huku ombi lake likipingwa.

Babu ametolea mfano wa Gavana wa Migori Okoth Obado anayehusishwa na mauaji ya Sharon Otieno na Sara Wairimu anayehusishwa na mauji ya mumewe Tob Cohen, ambao wameachiliwa huku Jowi akiendeleza kuzuiliwa.