array(0) { } Radio Maisha | Sijamtema Ruto kisiasa, asema Duale
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Sijamtema Ruto kisiasa, asema Duale

Sijamtema Ruto kisiasa, asema Duale

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Aden Duale amesema hakuna muda wa kutosha kuifanyia katiba marekebisho, akipendekeza sheria zilizopo kurekebishiwia bungeni.

Duale amesema licha ya kwamba bunge lina uwezo wa kuirekebisha katiba, hakuna muda uliowekwa kwa shughuli hiyo kufanywa kwani rais wa taifa lolote lile anaweza kukosa kutia saini mswada kwa wakati au hata kutupilia mbali kufuatia ukosefu wa muda wa kutosha.

Akizungumza jijini Kisumu wakati wa mkutano na viongozi wa Chama cha Wahariri, Editors Guild, Duale amesema hakuna sheria iliyobuniwa kwamba ni lazima katiba ifanyiwe marekebisho kwa kipindi fulani huku akinukuu kifungu cha 256 (5) cha katiba.

 

Kauli yake inajiri huku viongozi wa upinzani na baadhi ya walioko serikalini wakishinikiza katiba kufanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo ili kufanikisha usawa.

Wakati uo huo,

Duale amepuuza madai kwamba amemtema kisiasa Naibu wa Rais Daktari William Ruto akisema yeye si kibaraka wa yeyote kisiasa.

Akizungumza na wanahabari, Duale amepuuza taarifa kuwa amevunja uhusiao baina yake na Ruto.

Pamekuwapo na tetesi kuwa wawili hao wametofautiana kuhusu shinikizo la kuifanyia katiba marekebisho, ambapo Duale anapendekeza mfumo wa uongozi wa bunge huku Ruto akiupinga

Duale aidha amewashauri wanahabari kutoegemea upande wowte wanapoandaa taarifa.