array(0) { } Radio Maisha | Wakenya wanane wakamatwa Rwanda kufuatia jaribio la wizi Equity Bank
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakenya wanane wakamatwa Rwanda kufuatia jaribio la wizi Equity Bank

Wakenya wanane wakamatwa Rwanda kufuatia jaribio la wizi Equity Bank

Watu kumi na wawili wamekamatwa nchini Rwanda kufuatia jaribio la wizi wa fedha katika Benki ya Equity. Wanane miongoni mwao ni Wakenya, watatu wakiwa raia wa taifa hilo huku mmoja akiwa raia wa Uganda.

Kwa mujibu wa Idara ya Uchunguzi nchini Rwanda, RIB kumi na wawili hao walikuwa wakitumia mtandao kushiriki wizi huo ila njama yao ikatibuliwa.

Kumi na wawili hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kudukua mtandao wa benki hiyo ili kuziiba pesa za wateja.

RIB imesema washukiwa wametekeleza jaribio hilo baada ya kufaulu kuiba pesa katika benki hiyo kwenye mataifa ya Kenya na Uganda.

Kisa hiki kinajiri miezi kadhaa baada ya Makachero wa Idara ya Upelelezi, DCI kumnasa mwanamme mwenye umri wa miaka ishirini na sita anayeaminiki kudukua akaunti za Equity na kuiba shilingi laki nne.

Katika siku za hivi karibuni, Wakenya wengi wamepatikana na hatia ya kushiriki uhalifu wa kimtandao, miongoni mwao wakiwa wanasiasa na wakuu serikalini.

Oktaba tarehe tatu, watu watatu walishtakiwa kwa tuhuma za kuiba shilingi zaidi ya laki tisa katika benki hiyo, fedha za ajuza wa miaka 67.