array(0) { } Radio Maisha | Waziri Tobiko anaongoza shughuli ya upanzi wa miche katika eneo la Sera Leone Msituni Mau
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Waziri Tobiko anaongoza shughuli ya upanzi wa miche katika eneo la Sera Leone Msituni Mau

Waziri Tobiko anaongoza shughuli ya upanzi wa miche katika eneo la Sera Leone Msituni Mau

Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko anaongoza shughuli ya upanzi wa miche katika eneo la Siera Leone katika Msitu wa Mau. Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Waziri Tobiko amesema asilimia 96 ya wakazi tayari wameondoka kwa ihari huku akisema shughuli yenyewe ilifanyika kwa kuzingatia haki za wakazi hao.

Tobiko amesisitiza kwamba waliokuwa wakiishi msituni Mau na ambao wamekaidi agizo la serikali la kuwataka waondoke watafurushwa, na kuwashtumu viongozi wa kisiasa wanaoikosoa shughuli hiyo kwa kudai kuwa mpango huo si wa serikali bali wa mtu binafsi.

Tobiko amesema katika awamu hii ya pili serikali inalenga kuzrejesha ekari ishirini na mbili za ardhi zilizokuwa zimenyakuwa hivyo kufikisha thelathini na tano ekari ambazo zitakuwa zimerejeshwa tangu kuanza kwa mpango wa kuwafurusha watu Mau.

Wakati uohuo, Waziri Tobiko amesema atashiriki mazungumzo na viongozi wengine ili kuamua iwapo wakazi ambao ni wakulima waliokuwa wamepanda mimea yao shambani wataruhusiwa kurejea kuivuna, huku akipuuza madai kuwa waliofurushwa ni wakimbizi akisema wanaishi kwenye ardhi za Mau kinyume na sheria.

Kando na upanzi huo wa Miti Waziri Tobiko amesema kutawekwa ua , vile vile mipaka ili kuwazuia watu kuingia katika msitu huo na kuharibu mazingira.