array(0) { } Radio Maisha | Mfumo duni wa uteuzi umechangia vijana kutengwa, amesema Anne Nderitu

Mfumo duni wa uteuzi umechangia vijana kutengwa, amesema Anne Nderitu

Mfumo duni wa uteuzi umechangia vijana kutengwa, amesema Anne Nderitu

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa imesema inashughulikia mwongozo utakaohakikisha kunakuwapo na uwazi na uwajibikaji katika mchakato wa kuwateua wagombea mbalimbali kwenye vyama vya kisiasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya ujumuishaji wa vijana na wanawake katika bunge la kumi na moja na kumi na mbili, Msajili wa Vyama Ann Nderitu amesema vijana na wanawake ambao ndio wengi nchini mara nyingi hutengwa katika uongozi kufuatia mfumo duni wa uteuzi wa wagombea.

Nderitu amesema tayari ofisi hiyo inashirikiana na baadhi ya wabunge kuandaa mswada wa sheria za uteuzi ambao utawasilishwa bungeni ili kujadiliwa na iwapo bunge litaupitisha basi vijana na wanawake watakuwa wakipata nafasi sawa na vijana katika nyadhifa za kisiasa.