array(0) { } Radio Maisha | KNHCR imewashauri washikadau mbalimbali kupigania haki za wanyonge

KNHCR imewashauri washikadau mbalimbali kupigania haki za wanyonge

KNHCR imewashauri washikadau mbalimbali kupigania haki za wanyonge

Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadamu KNHRC imewashauri washikadau wa sekta mbalimbali kushirikiana katika kupigania haki za wanyonge.

Tume hiyo imesema unyanyapaa, utepetevu wa maafisa wa uchunguzi, tamaduni zilizopitwa na wakati na ukosefu wa taarifa muhimu vimeathiri kuamuliwa kwa kesi za unyanyasaji.

Akizungumza katika eneo la Maralal kaunti ya Samburu, afisa wa tume hiyo Naomy Setiyo ameeleza haja ya serikali kuwawahasisha Wakenya dhidi ya ukeketaji miongoni mwa wasichana.

Setiyo amesema watoto wengi wanahangaika huku kesi za unyanyasaji zikikaa kwa muda mrefu mahakamani bila kuamuliwa hivyo kuchelewesha haki  kwa waathiriwa.

Setiyo vilvile amesikitia hali ambapo visa vya unajisi vinazidi kuripotiwa katika maeneo mbalimbali huku akiwasihi wazazi kuwalinda wanao msimu huu wa likizo.