array(0) { } Radio Maisha | Safaricom yarekodi faida ya shilingi bilioni 35.6
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Safaricom yarekodi faida ya shilingi bilioni 35.6

Safaricom yarekodi faida ya shilingi bilioni 35.6

Kampuni ya Safaricom imerekodi faida ya shilingi bilioni 35.6 katika kipindi cha nusu  mwaka huu wa kifedha. Fedha hizi ni sawa na asilimia 14.4 ya mauzo.

Ukuaji huu umechangiwa na kuongezeka kwa wateja wake wanaotumia bandali, kwa asilimia 43.6 huku idadi ya wanaotumia mtandao wa Safaricom ikiongezeka kwa asilimia 14.8. Aidha kuongezeka kwa wateja wanaotumia Huduma ya Kutuma na Kupokea pesa ya M-pesa wameongezeka kwa asilimia 12.4

Katika kipindi sawa na hicho mwaka uliopita, kampuni hiyo ilirekodi faida ya shilingi bilioni 31.5 sawa na asilimia 20.2 ya mauzo yake.

Aidha kampuni hiyo ilirekodi faida ya shilingi bilioni 19.5 sawa na asilimia 10.8 mwaka wa 2017.