array(0) { } Radio Maisha | Jaribio la Wambora kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri lapingwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Jaribio la Wambora kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri lapingwa

Jaribio la Wambora kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri lapingwa

Wawakilishi Wadi katika Bunge la Kaunti ya Embu wamepinga juhudi za gavana wa kaunti hiyo Martin Wambora kutaka kuwahamisha kwenye wizara nyingione maafisa wakuu katika wizara mbalimbali wanaokumbwa na kashfa za ufisadi.

Wakizungumza kwenye kikao cha kujadili mpango huo bungeni, Wawakilishi hao badala yake wamesisitiza kuwa ni sharti Gavana Wambora awatimue afisini maafisa hao na kuwateua wengine watakaoendelea kuwahudumia wakazi wa Embu.

Kulingana nao, Gavana anastahili kujitenga na maafisa wafisadi katika serikali yake ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kikamilifu kwa wakazi. Wamedai kuwa maafisa hao walifuja mamilioni ya pesa katika mpango wa matangazo licha ya mpango huo kuwekewa kiasi cha fedha. Sammy Muturi ni Mwakilishi wa Wadi ya Ruguru.

Katika kikao hicho wawakilishi hao aidha wameitaka Idara ya Upelelezi DCI na Tume ya Kukabili Ufisadi Nchini EACC kuwachunguza maafisa wakuu Ruth Ndirangu na Janes Ndegi kufuatia madai ya matumizi mabaya ya shilingi milioni mia tatu. Micheal Njeru ni Kiongozi wa Wengi katika bunge hilo.