array(0) { } Radio Maisha | Viongozi washauriwa kusitisha mijadala kuhusu BBI
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Viongozi washauriwa kusitisha mijadala kuhusu BBI

Viongozi washauriwa kusitisha mijadala kuhusu BBI

Huku Jopo la Upatanishi, BBI likitarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga, wakazi wa Kaunti ya Trans Nzoia wamewaomba viongozi kusubiri hadi ripoti hiyo itakapowekwa wazi kwa umma ili kuijadili hadharani kwa kuzingatia yaliyomo.

Mmoja wa wakazi hao, Emmanuel Wanyama amesema baadhi ya viongozi wameanza kutumia ripoti ya BBI kujipigia debe na kuendeleza siasa za kuwagawanya Wakenya.

Matamshi hayo yameungwa mkono na Vincent Sambirir ambaye amewahimiza viongozi wakati wa kulijadili suala la BBI kuzingatia Mkataba wa Amani wa Mabanga yaani Mabanga Peace Accord baina ya jamii zinazoisha kwenye Kaunti za Trans Nzoia na Bungoma ambao ulitilia mkazo ugavi sawa wa nyadhifa mbalimbali za uongozi miongoni mwa masuala mengine.

Mkataba wa Mabanga ulitiwa saini na jamii hizo mbele ya aliyekuwa Naibu wa Rais, Kalonzo Musyoka kwa lengo la kuimarisha umoja na utangamano miongoni mwa Wakenya.