array(0) { } Radio Maisha | Maseneta wapendekeza feri kutumika tena kuwavusha watu Likoni
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Maseneta wapendekeza feri kutumika tena kuwavusha watu Likoni

Maseneta wapendekeza feri kutumika tena kuwavusha watu Likoni

Kamati ya Seneti ya Uchukuzi sasa imependekeza Feri  ya Nyayo, Kilindini na Mv Harambee zisitumike tena katika shughuli ya kuwavusha watu katika kivuko cha Likoni-Ferry jijini Mombasa huku ikiitaka Idara ya Upelelezi DCI na Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi kuchunguza matumizi ya fedha katika Shirika la Huduma za Feri

Kamati ilitembelea Mamlaka ya Shughuli za Baharini KMA kuchunguza ajali ya mwezi jana iliyosababisha vifo vya Mariam Kigenda na mwanawe Amanda Mutheu.

Katika ripoti iliyowasilishwa na Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, usimamizi wa Shirika la Huduma za Feri ulishtumiwa kufuatia kuwapo kwa Feri zisizo afikia viwango  zinazoendelea kuhudumu katika kivuko hicho. Aidha ripoti hiyo ililishtumu shirika hilo ikisema kuwa iwapo Feri hiyo ingekuwa katika hali nzuri ajali hiyo haingetokea.

Aidha inadaiwa kuwa mamilioni ya fedha zilitumika kuzikarabati feri hizo huku Meneja Mkurugenzi a shirika la KFS Bakari Gowa akiwa na wakati mgumu kujieleza mbele ya kamati hiyo ni kwa nini baadhi ya feri zinazohudumu ni chakavu licha ya idadi kubwa ya wakenya kutegemea huduma hizo kila uchao.

Hata hivyo Wizara ya Uchukuzi imesema inahitaji fedha zaidi ili kuzikarabati Feri hizo licha ya KFS kupendekeza baadhi kuondolewa kwa kuwa zimehudumu kwa zaidi ya miongo miwili hali ambayo huenda ikahatarisha zaidi maisha ya Wakenya.