array(0) { } Radio Maisha | Afisa wa Kitengo cha GSU akiri kutekeleza mauaji

Afisa wa Kitengo cha GSU akiri kutekeleza mauaji

Afisa wa Kitengo cha GSU akiri kutekeleza mauaji

Afisa wa Kitengo cha GSU anayetuhumiwa kuwaua wanawake wawili kwenye eneo la Katani Kaunti ya Machakos amekiri kutekeleza mauaji hayo.

Anthony Kilonzo amefikishwa mahakamani leo hii ambapo amekiri kuwaua Peared Purity Wanjiru, mwenye umri wa miaka thelathini na mitano na mamaye Anne Gatiti, mwenye umri wa miaka sitini baada ya kuhojiwa.

Hata hivyo, mahakama imemzuia kuendelea kukiri akisema alihitaji wakili. Mahakama imeagiza azuiliwe kwa siku ishirini na moja zaidi katika kituo cha Polisi cha Kilimani.

Wakati uo huo ameagiza mshukiwa afanyiwe uchunguzi wa kiakili kabla ya kurejeshwa tena mahakamani.

Kilonzo ni miongoni mwa washukiwa wanne waliokamawa kufuatia mauaji hayo yaliyotekelezwa Jumamosi iliyopita.

Ikumbukwe jana maafisa wa polisi walimuua mshukiwa mwingine wa mauaji hayo.