array(0) { } Radio Maisha | ODM yakataa kutambua sajili ya wapigakura

ODM yakataa kutambua sajili ya wapigakura

ODM yakataa kutambua sajili ya wapigakura

Chama cha ODM imekataa kutambua sajili ya wapigakura ya uchaguzi mdogo wa Kibra ambayo imetolewa na Tume ya Uchaguzi IEBC, kikisema haijakamilika.

Chama hicho kimesema sajili hiyo ambayo imetolewa kwa umma haina nambari za watu za vitambulisho, hatua ambayo imetatiza shughuli za kuwatambua wapigakura.

ODM sasa imetoa wito kwa IEBC kuwasilisha sajili nyingine yenye majina kamili ya wapigakura, vituo vya kupigakura na nambari zao wa vitambulisho. Tume hiyo awali ilisema kwamba ilikuwa imetoa sajili kamili yenye maelezo yote kwa ajili ya uchaguzi huo.

Kupitia taarifa rasmi Oktoba 25, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema tume hiyo imekamilisha shughuli zote za maandalizi ya uchaguzi huo. Takribani watu alfu mia moja kumi nane, mia sita sitini na nane, wamesajili kushiriki uchaguzi huo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa ,Ken Okoth mwaka huu. Wagombea ishirini na wanane watashiriki uchaguzi huo.