array(0) { } Radio Maisha | Bunge la Kitaifa limesifiwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Bunge la Kitaifa limesifiwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili

Bunge la Kitaifa limesifiwa kwa kutafsiri kanuni za kudumu za Bunge kutoka lugha ya Kiingereza hadi Kiswahili. Spika wa Bunge la Tanzania Job Yustino Lughai, amesema hatua hiyo inatoa nafasi kubwa sana kwa mataifa ya Afrika Mashariki kushirikiana na kuwasiliana kwa urahisi.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Kamati za Bunge la Kitaifa, Lughai amesema inasikitisha kuona mataifa ya Afrika yakizipuuza lugha asili na kuzienzi zile za mataifa hasa ya yaliyoyatawala. Amesema inawezekana kwa mabunge hasa ya mataifa ya Afrika Mashariki kutumia lugha ya Kiswahili kwa mawasiliano.

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi kwa upande wake amesema kwamba, chini ya uongozi wake Bunge la kumi na mbili limepiga hatua kubwa katika mageuzi si tu kwa kuchapishwa kwa kanuni hizo bali pia kupitishwa kwa miswada mbalimbali vilevile utumiaji wa teknolojia.

Viongozi wengine wa bunge wakiunga mkono kauli hiyo ya Spika wamesema watazidi kuwashinikiza wenzao hasa katika kamati za bunge kuyatekeleza majukumu yao ifaavyo. Adan Duale ni Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa.

Awali Aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Francis Ole Kaparo amewashuri wabunge kujiepusha na ufisadi akisema umeathiri pakubwa maendeleo nchini.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Kaparo amesema Bunge la Kitaifa limepiga hatua tangu Kenya kujinyakulia uhuru na wabunghe wanastahili kuhakikisha linasonga mbele bila kuathirika na utendakazi duni, uzembe na ufisadi.

Wakati uo huo, kuanzia leo hii vikao vya kamati zote za bunge vitakuwa vikipeperushwa moja kwa moja jinsi ilivyo kwa vikao vya Bunge la Kitaifa na Seneti.

Aidha, ripoti mbalimbali za kamati zote za bunge zitazinduliwa leo hii ili kuonesha hatua zilizopigwa na bunge hilo kufikia sasa.

. Spika wa Bunge la Tanzania Job Yustino Lughai, amesema hatua hiyo inatoa nafasi kubwa sana kwa mataifa ya Afrika Mashariki kushirikiana na kuwasiliana kwa urahisi.