array(0) { } Radio Maisha | Al-Shabaab wakiri kutekeleza shambulio, Wajir

Al-Shabaab wakiri kutekeleza shambulio, Wajir

Al-Shabaab wakiri kutekeleza shambulio, Wajir

Kundi la kigaidi la Al-Shaabab limekiri kuhusika katika shambulio katika Kituo cha Polisi cha Dadajabula kwenye Kaunti ya Wajir, usiku wa kuamkia leo.

Inaarifiwa kwamba wanakundi hao waliokuwa wamejihami vikali walikivamia kituo hicho kilicho kilomita 13 kutoka mpaka wa Somalia na Kenya na kwamba shambulio lao lililenga kuwakomba wenzao wawili ambao wamekuwa wakizuiwa kituoni humo.

Aidha, wakati wa makabiliano hayo yaliyodumu tariban nusu saa, maafisa watatu wa polisi wa utawala walijeruhiwa huku wanakundi wawili wa Al Shabaab wakiuliwa.

Vilevile, hakuna silaha iliyoibiwa wakati wa tukio hilo la usiku wa kuamkia leo.