array(0) { } Radio Maisha | Ndege ya Safarilink yapasuka gurudumu
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Ndege ya Safarilink yapasuka gurudumu

Ndege ya Safarilink yapasuka gurudumu

Katika misururu ya visa vya ajali za ndege nchini, ndege ya kampuni ya Safarilink iliyokuwa imeratibiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Wilson kutoka Kisiwa cha Lamu ilipasuka gurudumu lake wakati wa kutua.

Usimamizi wa kampuni hiyo umethibitisha kisa hicho cha jana jioni ikisema kwamba kupasuka kwa gurudumu hilo kuliifanya ndege hiyo yenye usajili 5Y-SLJ kupoteza mwelekeo na kuondoka nje ya barabara.

Hata hivyo, abiria wote 10 waliokuwemo na wafanyakazi wawili wa Safarilink hawakujeruhiwa wakati wa tukio hilo.

Kisa hiki kimejiri siku moja tu baada ya ndege ya Kampuni ya Silverstone k kutua ghafla kufuatia hitilafu kwenye mojawapo ya magurudumu yake.

Ndege hiyo ambayo ilikuwa ikipaa kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Eldoret kuelekea Lodwar, ililazimika kutua ghafla baada ya mojawapo ya gurudumu lake upande wa kushoto kung'oka.

Hata hivyo, hakuna aliyejeruhiwa wakati wa tukio hilo.

Aidha, wiki tatu zilizopita, abiria hamsini na watano akiwamo rubani walinusurika kifo baada ya ndege ya kampuni hiyo ya Silverstone waliyokuwa wameabiri kuanguka dakika chache tu baada ya kupaa katika Uwanja wa Ndege wa Wilson.