array(0) { } Radio Maisha | Wakuu wa KNUT waafikiana kusitisha mgogoro baina yao
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Wakuu wa KNUT waafikiana kusitisha mgogoro baina yao

Wakuu wa KNUT waafikiana kusitisha mgogoro baina yao

Na Caren Omae,

NAIROBI, KENYA, Hatimaye maafisa wa Chama cha Kitaifa cha Walimu KNUT wameafikiana kusitisha mgogoro baina yao na badala yake kushirikiana.

Wakizungumza katika kikao kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi COTU Francis Atwoli, maafisa hao wamesema wameyazungumzia masuala ambayo yalikuwa yakiibua utata na kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja. Atwoli amesema maafikiano hayo yalikuwa ya ihari na hakuna aliyeshinikizwa.

Katibu Mkuu wa KNUT Wilson Sossion amesema mvutano huo ulikuwa umeathiri pakubwa utendakazi wake kutokana na mwingilio.

Sossion aidha amesema KNUT imeahirisha mkutano wa Baraza Kuu la Chama uliotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, hadi mwaka ujao. Amesema hatua hiyo ni kutokana na kutokuwapo na maandalizi ya kutoasha katika matawi ya chama hicho kote nchini.

Amewahakikishia wanachama wake kwamba masuala yote yameshughulikiwa na kwmaba kesi zote zilizokuwa mahakamani zitaondolewa.

Wakati uo huo, amekana madai kwamba kuna mvutano baina ya KNUT na Wizara ya Elimu huku akisema wataendelea kushirikiana na idara hizo muhimu kwa manufaa ya Walimu.

Ametoa wito kwa TSC kuyashughulikia masuala ya walimu walioathirika wakati wa mpango wa kutathimini utendakazi wa walimu huku akiitaka kuwarejesha kazini wote waliofutwa. Aidha ameitaka TSC kukoma kuingilia mishahara ya walimu.

Ikumbukwe shughuli katika ofisi za KNUT zilikuwa zimekwama kwa muda kufuatia mgogoro baina ya Sossion na wanachama wengine walotaka kumwondoa katika wadhfa wake. Sossion alishtumiwa kwa kuendelea kushikilia wadhfa wa katibu mkuu licha ya kuwa Mbunge, hivyo kukiuka sheria za chama.