array(0) { } Radio Maisha | Mvua kundelea kunyesha katika maeneo ya Kaskazni Mashariki, Bonde la Ufa na Pwani
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mvua kundelea kunyesha katika maeneo ya Kaskazni Mashariki, Bonde la Ufa na Pwani

Mvua kundelea kunyesha katika maeneo ya Kaskazni Mashariki, Bonde la Ufa na Pwani

Huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha vifo vya takribani watu kumi kufikia sasa, Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imeonya kwamba mvua hiyo itandelea katika maeneo ya Kaskazni Mashariki, Bonde la Ufa na Pwani.

Idara hiyo imesama kwamba mvua kubwa itakayoandamana na mafuriko itanyesha hadi Juma tano katika  Kaunti za Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa, Isiolo, Nairobi, Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang'a, Kiambu, Meru, Embu, Tharaka Nithi, Turkana, West Pokot na Samburu.


Kaunti zingine ni pamoja na Kitui, Makueni, Machakos, Kajiado, Taita Taveta,  Mombasa, Tana River, Kilifi, Lamu na Kwale.
Mkurugenzi wa idara hiyo Stella Aura, amesema upepo mkali utakaovuma kwa kasi ya knoti  25 itavuma katika maeneo ya Kaskazini Mashariki na Maghari kwa kipindi cha wiki moja.


Takribani watu alfu moja wameachwa bila makao huku idara yenyewe ikiwataka Wakenya wanaoishi katika maeneo yanayoweza kukumbwa na maporomoko na mafuriko kuhamia maeneo salama.

Wakulima katika  Kaunti za Turkana, Wajiri na Marsabit miongoni mwa nyingine, wamepata hasara baada ya mufigo wao kusomwa na mvua kubwa tangu Juma liliopita.