array(0) { } Radio Maisha | Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefunguliwa baada ya kufungwa

Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefunguliwa baada ya kufungwa

Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefunguliwa baada ya kufungwa

Chuo Kikuu cha Kenyatta kimefunguliwa baada ya kufungwa kwa muda tarehe saba mwezi huu wa Oktoba kufuatia maandamano ya  wanafunzi wakilalamikia madai ya uongozi mbaya wa chuo hicho.


Aidha shughuli za masomo kwa wanaosomea taaluma ya Udaktari, Uuguzi, Uhandisi na Teknolojia vilevile Ujenzi na Mazingira yataanza kesho Oktoba ishirini na mbili, wanafunzi wakitakiwa kuripoti shuleni leo hii.


Katika barua iliyotumwa kwa Wakuu wa Idara mbalimbali chuoni humo, masomo ya Kilimo Biashara, Uanahabari, Ubunifu na Masuala ya Utaliii wametakiwa kuripoti chuoni humo kesho Jumanne kabla ya kuanza masomo yao Jumatano.


Aidha wanafunzi wa taaluma ya Ualimu na Sayansi ya Kijamii wataripoti Jumatano kisha kuanza masomo siku ya Alhamisi. Wanafunzi wanaosomea katika bawa kuu wametakiwa kulipa faini ya shilingi mia tano kufuatia hasara waliyosababisha wakati wa maandaamo.

Ikumbukwe wanafunzi hao waligoma na kusabambisha msongamano wa magari katika barabara kuu ya Thika wakimtaka Naibu Mkuu wa chuo hicho Profesa Paul Wainaina kujiuzulu kufuatia madai ya kuendeleza dhuluma kwa wanafunzi chuoni humo.