array(0) { } Radio Maisha | Walinzi wa Kampuni ya Maua wanamzuilia mwanahabari wa Shirika la Habari la Standard

Walinzi wa Kampuni ya Maua wanamzuilia mwanahabari wa Shirika la Habari la Standard

Walinzi wa Kampuni ya Maua wanamzuilia mwanahabari wa Shirika la Habari la Standard

Walinzi wa Kampuni ya Maua ya Finlays mjini Kericho wanamzuilia mwanahabari wa Shirika la Habari la Standard aliyekuwa amefika katika kiwanda hicho kufuatia taarifa inayohusu kiwanda hicho.

Mwanahabari Nikko Tanui, ambaye alikuwa ameandamana na  Dickson Sang amabye ni afisa idara ya Kilimo katika kaunti hiyo, walikuwa wanafuatilia taarifa kuhusu tangazo la Kampuni ya Finlays kufunga mashamba yake ya maua ya Chemirei na Tarakwet.

Ikumbukwe kwamba Meneja Mkuu wa Finlays Stephen Scott,  Oktoba 19  alitangaza kwamba kampuni hiyo ingefunga mashamba yake mawili ya maua mapema kinyume na ilivyokuwa imewatangazia wafanyakazi. Shughuli hiyo itasababisha wafanyakazi 1,100 kukasa nafasi za ajira.

Mwanahabari huyo amesema kwamba hajaarifiwa ni kwanini amezuiliwa na walinzi huku walinzi wenyewe wakiendelea kuwapigia simu wakubwa wao kuhusu kunaswa huko