array(0) { } Radio Maisha | Mackdonald Mariga ahidi kujenga shule Kibra
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mackdonald Mariga ahidi kujenga shule Kibra

Mackdonald Mariga ahidi kujenga shule Kibra

Huku uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Kibra ukiendelea kukaribia, Mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Jubilee Mackdonald Mariga ameahidi kujenga shule moja ya umma katika kila wadi endapo wakazi hao watamchagua kuwa mbunge wao.

Akuzungumza wakati wa kuwakabidhi watahiniwa wa darasa la nane katika eneo hilo vifaa vya kufanyia mtihani wa KCPE, Mariga amesema shule hizo zitajengwa katika muda wa mwaka mmoja. Aidha kuhusu suala la namna Fedha za Hazina ya Basari zitakavyogawanyiwa wanafunzi, Mariga amesema atalibuni Jopo Maalum litakalowajumuisha wazazi na Walimu katika kila wadi.

Wakati uo huo,  amesema kuwa atarejesha mpango wa chakula kwa wanafunzi katika shule za umma ambao utafadhiliwa na wakfu wake. Amesema atahakikisha kuwa serikali ya jubilee inaongeza idadi ya vyuo vya kiufundi katika eneo hilo kwa muda wa mwaka mmoja, ili kutoa fursa kwa vijana kupata ujuzi katika taaluma mbalimbali.

Hata hivyo Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi yuko Kibra kumpigia debe mwaniaji wa kiti hicho kwa chama chake Eliud Owalo wakati Amisi Buti wa FordKenya akifanya kampeni zake nyumba kwa nyumba.

Jumla ya wagombea kumi na watano wanawania kiti hicho katika uchaguzi ambao utafanyika mnamo Novemba saba